Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti
ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo
wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi
tulio hai wakati huo tutakusanywa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana
hewani. Na hivyo tutakuwa daima pamoja na Bwana. Basi, farijianeni kwa
maneno haya.
1 Thessalonians 4 : 16 -
18
Sikilizeni, nawaambieni siri: sisi hatutakufa sote,
ila sote tutageuzwa wakati wa mbiu ya mwisho, kwa nukta moja, kufumba na
kufumbua. Maana mbiu itakapolia, wafu watafufuliwa katika hali ya kutoweza
kufa tena, na sisi tutageuzwa.
1 Corinthians 15 : 51 - 52
Ndugu, hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya nyakati
na majira yatakapotukia mambo haya. Maana ninyi wenyewe mwajua kwamba Siku
ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. Watu watakapokuwa wanasema: "Kila
kitu ni shwari na salama" ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo
hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua,
wala watu hawataweza kuepukana nayo. Lakini ninyi ndugu, hamko gizani,
na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi.
1 Thessalonians 5 : 1 - 4
Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala
pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa. Wanawake wawili watakuwa
wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa." Watu
wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Hapo
wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai
watakapokusanyikia."
Luke 17 : 34 - 37